OBAMA ATUA ETHIOPIA

OBAMA ATUA ETHIOPIA

Like
240
0
Monday, 27 July 2015
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama hatimaye amefika nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya kuzitembelea baadhi ya nchi za Afrika.

Imeelezwa kuwa hiyo ni mara yake ya kwanza tangu aongoze Taifa la Marekani akiwa rais kuhutubia wanachama 52 wa umoja wa Afrika katika makao makuu yaliyoko Addis ababa nchini Ethiopia.

Hata hivyo Mazungumzo yao yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini sudan ya kusini ambapo Rais Obama amewasili nchini Ethiopia akitokea mjini Nairobi.

Comments are closed.