OBAMA AWASILI ZIARANI BEIJING

OBAMA AWASILI ZIARANI BEIJING

Like
359
0
Monday, 10 November 2014
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amewasili mjini Beijing,China hii leo ambako yuko katika ziara itakayomfikisha katika nchi tatu za Asia na Pacifiki.

Obama yuko nchini humo kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nchi za Asia na Pacifiki, APEC ambao unahudhuriwa pia na viongozi wengine wa nchi akiwemo Rais wa Urusi Vladimir Putin na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Rais Obama atafanya mazungumzo na rais mpya wa Indonesia Joko Widodo na waziri mkuu wa Australia Tony Abbott. Mkutano huo wa APEC unaozikutanisha pamoja nchi wanachama 21 unatarajiwa kuhitimishwa hapo kesho.

OBAMA2

Comments are closed.