OBAMA: TRUMP HATAKUWA RAIS

OBAMA: TRUMP HATAKUWA RAIS

Like
227
0
Wednesday, 17 February 2016
Global News

RAIS Barack Obama wa Marekani amesema  anaamini mgombea urais wa Chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani.

Bwana Trump, Mfanyabiashara tajiri kutoka New York, anaongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea wa chama cha Republican na tayari ameshindakatika Uchaguzi wa mchujo jimbo moja.

Akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa Kiuchumi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California, alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wa Habari Mmoja kumuuliza swali lililomhusu Trump.

Comments are closed.