OBI MOBILE YADHAMIRIA KUSAMBAZA TEKNOLOJIA KUKUZA UCHUMI NCHINI

OBI MOBILE YADHAMIRIA KUSAMBAZA TEKNOLOJIA KUKUZA UCHUMI NCHINI

Like
259
0
Friday, 27 February 2015
Local News

KAMPUNI ya simu ya Obi mobiles imedhamiria kusambaza teknolojia kwa watu  wengi zaidi nchini Tanzania lengo ikiwa ni kufanya utendaji wenye tija katika vifaa vya simu za mkononi  kwa maendeleo ya nchi na kusaidia kukuza uchumi.

Hayo yamebainishwa na mwanzilishi ambaye pia ni mkurugenzi  mtendaji wa zamani wa Apple, John Sculley, ambapo amesema kampuni hiyo inalenga kuongeza mauzo kupitia mpango mkakati unaowalenga vijana na watumiaji wanaokwenda na wakati na  matumizi ya simu za mkononi.

Kampuni ya Obi mobiles imezindua aina saba za simu  ambazo ni Hornbill S551,Falcon S 451,Crane S550,Wolverine S501,Fox S453,Racoon S401 na power GO F 240 kwa ajili ya soko la Tanzania na zina nafasi nzuri na uwezo wa internet.

 

Comments are closed.