OLIMPIKI: UCHAFU NI KIKWAZO KATIKA FUKWE ZA RIO DE JANEIRO

OLIMPIKI: UCHAFU NI KIKWAZO KATIKA FUKWE ZA RIO DE JANEIRO

Like
333
0
Thursday, 30 July 2015
Slider

Rais wa Kamati kuu ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach, amesema kuwa uchafuzi wa bahari ni moja ya kikwazo Rio de Janeiro katika maandalizi ya michuano ya hapo mwakani.

Hata hivyo kutokana na hali hiyo waandaji wa mashindano hayo ya riadha wamesema kuwa watafanya kila linalowezekana kwa afya ya wanariadha wakati wa Olympiki.

Takribani asilimia 70 ya maji taka yanamwagika Rio de Janeiro katika fukwe za Guanabara,eneo ambalo wapiga mbizi watafanyia mashindano yao.

Katika hali inayoonyesha ni hatari kwa afya wanariadha walioko kwenye mafunzo katika pwani hiyo wameona mizoga ya wanyama na uchafu ukiwa ukingoni mwa eneo hilo ambalo mashindano hayo yatafanyika.

Comments are closed.