ONGEZEKO LA MIFUGO LACHANGIA UKOSEFU WA MAJI KISHAPU SINYANGA

ONGEZEKO LA MIFUGO LACHANGIA UKOSEFU WA MAJI KISHAPU SINYANGA

Like
345
0
Tuesday, 07 April 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa, kuongezeka kwa Mifugo katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinganya,ni mojawapo ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa tatizo la Maji katika Wilaya hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Diwani wa Kata ya Ukenyenge, MAKANASA KISHIWA, amesema kuwa ili kuhakikisha tatizo la Maji linakwisha wameweza kuchimba Mto umbali wa Kilometa 15 kutoka Shinyanga na wataweza kusambaza Maji hayo.

KISHIWA amesema kuwa, wamekuwa wakikaa vikao vya Kata kuweza kuzuia Wanakijiji kupeleka Mifugo katika vyanzo vya maji, lakini wamekuwa wakikaidi hivyo kupelekea kuendelea kuteseka kwa kushindwa kupata huduma hiyo muhimu.

Comments are closed.