OPERESHENI YAKUPAMBANA NA MAJAMBAZI SUGU YAANZA TEMEKE

OPERESHENI YAKUPAMBANA NA MAJAMBAZI SUGU YAANZA TEMEKE

Like
338
0
Monday, 10 November 2014
Local News

JESHI la polisi Mkoa wa kipolisi Temeke wameanza kufanya operesheni mbalimbali za kupambana na majambazi sugu pamoja na kuondoa vyanzo vya uhalifu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.

 

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi  Temeke RPC Kihenya kihenya alipokuwa akizungumza na kituo hiki kuhusiana na changamoto za uhalifu zinazokuwa zinatokea katika kuelekea mwisho wa mwaka.

 

Mbali na hilo Kamanda Kihenya amesema kuwa kuna taarifa zinazotolewa na wananchi kuhusiana na utekeji wa watoto kwa kutumia magari aina ya Noah katika mkoa huo hazina ukweli wowote licha  ya jeshi hilo kuendelea na uchunguzi wa kina.

 

Comments are closed.