OTAMENDI NDANI YA MAN CITY

OTAMENDI NDANI YA MAN CITY

Like
215
0
Friday, 21 August 2015
Slider

Beki wa timu ya taifa ya kandanda Argentina, Nicolas Otamendi, amesaini na miamba wa Uingereza, Machester City, timu hiyo imetangaza Alhamisi kufuatia makubaliano na Valencia wa Uhispania kukamilisha biashara hiyo.

Otamendi, 27, amekubali kandarasi ya urefu wa miaka mitano ingawa dau husika halikutangazwa.

City wameimairisha ngome yao na Otamendi ambaye ataungana tena na mwenzake wa zamani katika majitu wa Ureno, FC Porto, Eliaquim Mangala na ndugu yake kwenye kikosi cha Argentina, Martin Demichelis pamoja na nahodha Vincent Kompany wa Ubelgiji.

“Niko hapa kupeana uwezo wangu wote, kupigana mechi baada ya mechi na kusukuma City kufikia nguzo za juu zaidi kwa kipindi kirefu inavyowezekana na natamani kunyakua mataji kadhaa pamoja na vikombe,” Otamendi alinukuliwa akisema na tovuti rasmi la timu hiyo inayoongoza jedwali la mapema la ligi Premier baada ya kushinda mechi mbili za mwanzo mtawalia na idadi ya mabao 3-0.

“Hilo ndilo muhimu zaidi. Kuwa ndani ya klabu hiki ambacho kutoka nje, kina mvutio mkubwa sana na ni ndoto kwangu,” aliendelea.

Valencia wanaaminika kutumia mauzo ya beki huyo kulipa kipande cha dau ambacho wanadaiwa na City kwa mshambuliaji Alvaro Negredo.

Comments are closed.