OUTTARA ASHINDA UCHAGUZI IVORY COAST

OUTTARA ASHINDA UCHAGUZI IVORY COAST

Like
224
0
Wednesday, 28 October 2015
Global News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Ivory Coast imemtangaza Alassane Ouattara kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo kwa ushindi wa asilimia 83.66.

Raia wa Ivory Coast wameonesha kufurahishwa na ushindi wa Rais Alassane Outtara kama walivyotarajiwa kwamba rais huyo ataongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Baada ya mwongo mmoja wa kutoimarika kwa uchumi na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wengi watafurahia kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa Amani.

Comments are closed.