OXFAM YATAKA MATAIFA YA AFRIKA MAGHARIBI YALIYOATHIRIWA NA EBOLA YASAIDIWE KIFEDHA

OXFAM YATAKA MATAIFA YA AFRIKA MAGHARIBI YALIYOATHIRIWA NA EBOLA YASAIDIWE KIFEDHA

Like
261
0
Tuesday, 27 January 2015
Global News

SHIRIKA la misaada la Oxfam limetoa wito wa kutolewa kwa msaada wa thamani ya mamilioni ya dola kusaidia nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na Ebola, mradi huu wa msaada unaitwa Marshall Plan.

Zaidi ya Watuelfu 8,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola, wengi wao nchini Sierra Leone,Guinea na Liberia. Mradi wa Marshall ulitumika baada ya vita ya pili ya Dunia kwa ajili ya kuwanusuru waathirika barani Ulaya.

Oxfam imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuridhia mpango wa utoaji misaada kutoka kwa nchi tajiri. Shirika hilo limesema msaada wa fedha unahitajika katika maeneo matatu-kuchangia pesa kwa Familia za waaathirika wa Ebola, kuwekeza katika kazi pia kusaidia kutoa elimu kuhusu maswala ya kiafya, elimu na usafi.

 

 

Comments are closed.