PAKISTAN: 260 WAPOTEZA MAISHA KWA TETEMEKO LA ARDHI

PAKISTAN: 260 WAPOTEZA MAISHA KWA TETEMEKO LA ARDHI

Like
175
0
Tuesday, 27 October 2015
Global News

Makundi ya uokoaji yanaendelea na juhudi za kuyafikia maeneo ya Kaskazini mwa Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan, ili kuwaokoa watu wanodhaniwa kuwa wameathirika na tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo hilo jana.

Hadi sasa imeelezwa kuwa zaidi ya watu 260 wamefariki, kutokana na tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea tangu kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Hata hivyo baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi nchini Afghanistan, yanadhibitiwa na wanamgambo wa Taliban, na kusababisha hali kuwa ngumu ya uokoaji.

Comments are closed.