PAKISTAN YANYONGA WAFUNGWA WENGINE TISA

PAKISTAN YANYONGA WAFUNGWA WENGINE TISA

Like
360
0
Wednesday, 18 March 2015
Global News

PAKISTAN imewanyonga wafungwa wengine tisa wauaji na kuifikisha idadi ya walionyongwa katika kipindi cha siku mbili zilizopita kufikia 21 nakufikisha idadi ya watu 48 walio nyongwa katika mkoa wa Punjab tangu Pakistan iliporejesha adhabu ya kifo mwezi Desemba mwaka jana.

Hatua hiyo imelaaniwa na Umoja wa Ulaya ambao unapinga adhabu ya kifo na katika taarifa yake umetoa wito wa kufutwa adhabu hiyo kote duniani.

Katika taarifa yake Human Rights Watch imesema walionyongwa leo ni pamoja na Mohammad Afzal ambaye wakati alipohukumiwa kifo alikuwa na umri wa miaka 16.

 

Comments are closed.