RAIS WA MAMLAKA ya ndani ya Wapalestina MAHMOUD ABBAS amesema Wapalestina watawasilisha tena kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa azimio litakaloiwekea Israel muda wa miaka mitatu kuondoka katika maeneo ya Wapalestina.
Azimio hilo limekataliwa wiki iliyopita huku wanachama Nane kati ya 15 wa Baraza la Usalama wakipiga kura kuliunga mkono.
Akizungumza katika ufunguzi wa maonesho kuhusu mji wa Jerusalem mjini Ramallah Rais ABBAS amesema hawajashindwa katika baraza la usalama, bali baraza hilo ndilo lililoshindwa kutimiza wajibu wake kwa Wapalestina.