Palestina na Israel zatatiza UN

Palestina na Israel zatatiza UN

Like
634
0
Wednesday, 14 November 2018
Global News

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kukubaliana na mwenendo wa ghasia zilizotokea hivi karibuni kati ya Israel na Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour ameilaumu Marekani kwa kuwa kipingamizi.

Mapigano makali kuwahi kutokea katika kipindi cha muda wa miaka minne, yaliibuka siku ya Jumapili iliyopita baada wa wapiganaji wa Hamas kuingilia kati operesheni za siri zilizokuwa zikifanywa na Israel katika ukanda wa Gaza.

Chama cha Wapalestina cha Hamas kimesema kinachunguza kama Isreael imezingatia makubaliano ya Misri ya kusitisha mapigano.

Kwa upande wake Israel nayo imesema itaendelea na mashambulio yake ya anga katika ukanda wa Gaza ikiwa ni lazima kufanya hivyo.

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon amesema nchi yake kila siku inafanya kila liwezalo kuhakikisha usalama wa watu wake.

”..Tunachukua hatua kuwalinda watu wetu. Na wakati unapojua kwamba kuna mtu anachimba njia ya chini ya ardhi ama kuna mtu anapanga mashambulizi ama tukio la utekaji, utachukua hatua za kujilinda.

Tutaendelea kuchujua hatua hizo, haijalishi zitafanyika wapi kwa ajili ya kuwalinda watu wetu na mashambulizi yajayo…” Amesema Danon

Katika mapigano hayo Wapalestina sita waliuawa na mashambulizi yaliyofanywa na Israel, huku roketi zilizorushwa na wapiganaji wa Hamas zikiua muisrael mmoja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *