PANGANI: SERIKALI YATOA MIEZI 3 KWA WALIOHODHI VIWANJA KUVIENDELEZA

PANGANI: SERIKALI YATOA MIEZI 3 KWA WALIOHODHI VIWANJA KUVIENDELEZA

Like
256
0
Wednesday, 06 January 2016
Local News

SERIKALI wilayani Pangani imewapa miezi mitatu baadhi ya watu waliohodhi viwanja vikiwemo vile vilivyopo pembezoni mwa bahari ya hindi kuviendeleza la sivyo haitasita kuwanyang’anya kwa mujibu wa sheria ili kuendeleza mji wa pangani ambao sehemu kubwa ya makao makuu ya wilaya imezungukwa na mapori.

Akizungumza na efm kuhusu baadhi ya wafanyabiashara kuhodhi maeneo kwa makusudi kwa lengo la kuyafanyia biashara, mkuu wa wilaya ya pangani Regina Chonjo amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani kwa kushirikiana na afisa ardhi kuanza haraka kufanya tathmini ya viwanja ambavyo havijaendelezwa ili sheria ianze kuchukua mkondo wake.

Comments are closed.