PAP HAINA UHUSIANO NA KIKWETE

PAP HAINA UHUSIANO NA KIKWETE

Like
327
0
Thursday, 13 November 2014
Local News

IMEELEZWA kuwa Kampuni ya PanAfrica Power Resources -PAP haina Mahusiano ya Umiliki na Familia ya Rais JAKAYA KIKWETE kama ilivyoainishwa kwa kuweka katika mitandao mbalimbali ya Kijamii.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Kampuni ya IPTL inayomilikiwa na PAP, JOSEPH MAKANDEGE alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na tuhuma hizo.

Hivi karibuni mtoto wa Rais JAKAYA KIKWETE, aitwaye MIRAJI KIKWETE alieleza kusikitishwa kwake na tuhuma hizo zinazotolewa dhidi yake kuhusishwa na umiliki wa kampuni ya PAP kwamba yeye na dada yake, SALAMA KIKWETE wanamiliki Asilimia 50 za PAP kupitia Simba Trust na kusema Siyo za kweli na ni Uzushi.

Comments are closed.