PAPA FRANCIS AANZA ZIARA AFRIKA

PAPA FRANCIS AANZA ZIARA AFRIKA

Like
245
0
Wednesday, 25 November 2015
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Francis ameondoka mjini Roma kuelekea nchini Kenya leo, ambako ataanzia safari yake barani Afrika itakayomfikisha pia nchini Uganda na katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Safari hiyo ya kwanza barani Afrika kufanywa na Papa huyo mwenye umri wa miaka 78 inatajwa kukabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama.

Ratiba ya ziara ya Kiongozi huyo  wa Kanisa katoliki duniani  ina mambo  mengi, yakiwemo kuutembelea mtaa wa mabanda nchini Kenya, madhabahu ya mashahidi wa kikristo nchini Uganda, na pia msikiti na kambi ya wakimbizi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Comments are closed.