IKIWA ni hatua ya kujumuisha umoja wa kikristo duniani, Kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki Ulimwenguni, Papa Francis amewaomba radhi waumini wa Kiprotestanti kutokana na unyanyasaji walioupata kutoka kanisa Katoliki miaka iliyopita.
Papa Francis amewataka waumini wa kanisa Katoliki pia kuwasamehe wale ambao waliwakosea ili wasiruhusu makosa yaliyotendeka kuwa sumu ya mahusiano ya sasa.
Kufuatia tamko hilo msemaji wa Vatcan ametangaza kuwa Papa Francis atazuru mji wa Lund uliopo Swedish eneo ambalo jumuiya ya Kilutheri ilianzishwa na kuanzisha dhehebu la Kilutheri karne tano zilizopita.