PAPA FRANCIS AREJEA MJINI ROME

PAPA FRANCIS AREJEA MJINI ROME

Like
324
0
Monday, 19 January 2015
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis  anarejea mjini Rome leo baada ya ziara ya wiki moja barani Asia ambako aliwavutia mamilioni ya watu na kuuwasilisha ujumbe wa kuwatetea  masikini.

Baba Mtakatifu alizitembelea Sri Lanka na Ufilipino katika ziara yake ya pili katika bara hilo, mnamo muda wa miezi mitano.

Hapo jana kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliongoza sala iliyohudhuriwa na waumini milioni sita katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila. Na katika ujumbe wake,Papa Francis kwa mara nyingine amewataka  watu waongeze juhudi ili kuuondoa umasikini.

 

 

Comments are closed.