PAPA FRANCIS ATAKASERA YA UHAMIAJI ULAYA

PAPA FRANCIS ATAKASERA YA UHAMIAJI ULAYA

Like
325
0
Wednesday, 26 November 2014
Global News

KIONGOZI  wa  Kanisa  Katoliki Papa  Francis  amelitaka bara  la  Ulaya  kutayarisha  sera  moja  na ya haki  katika suala la  uhamiaji.

Amesema mamia  kwa  maelfu  ya wahamiaji  wanaowasili  katika  mataifa  hayo kila  mwaka kupitia  baharini  wanahitaji  kukubalika na  msaada, na  sio kuwa  na  sera  zenye  maslahi  binafsi  ambazo zinahatarisha  maisha na  kuchochea  mzozo  wa  kijamii.

Papa Francis  ametoa  kauli hiyo  katika  bunge  la Ulaya  wakati  wa  ziara  fupi  iliyokuwa  na  lengo  la kuelezea  mtazamo  wake  kwa  Ulaya  robo  karne  baada ya  Papa John Paul  wa  pili  kuzuru  Strasbourg  na kulihutubia  bara  ambalo  bado  limegawanywa  na  pazia la  chuma.

 

Comments are closed.