KIONGOZI wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewaambia wanasiasa nchini Marekani kwamba wanapaswa kuwaangalia wahamiaji kama watu na sio idadi ya watu.
Katika hotuba yake ya dakika 50 , kiongozi huyo wa kanisa amegusia mzozo wa wakimbizi katika bara la Ulaya wakati akielezea kuhusu madhila ya mamilioni ya wahamiaji kutoka America ya kusini ambao wanafasiri kuelekea kaskazini kutafuta maisha bora.
Papa Francis ametoa wito wa kuondolewa kwa adhabu ya kifo na usawa wa kiuchumi kushughulikiwa.