KIONGOZI mkuu wa Kanisa Katoliki dunia Papa Francis amewataka viongozi wa kikristo na Kiislamu nchini Kenya kujadiliana juu ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kinyama ya Waislamu wa itikadi kali yalioikumba Kenya.
Papa Francis ameyasema hayo leo nchini humo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu kama sehemu ya ziara katika nchi tatu za kiafrika.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani amekutana na viongozi wa kidini mjini Nairobi kabla ya misa yake ya kwanza iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini akiwemo Rais Uhuru Kenyatta.