PAPA FRANCIS AZURU KITONGOJI CHA WATU MASIKINI KENYA

PAPA FRANCIS AZURU KITONGOJI CHA WATU MASIKINI KENYA

Like
247
0
Friday, 27 November 2015
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis leo asubuhi amezuru katika maeneo wanakaoishi watu maskini katika kitongoji cha Kangemi, Nairobi, ambapo ametoa kauli kali dhidi ya matajiri wachache wanaowatenga maskini wenye shida.

 

Amewakosoa matajiri hao kwa kuhodhi mali ambazo zingewasaidia maskini.

 

Akizungumza katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi, Papa Francis amesema amezuru kwenye eneo linalokaliwa na watu wapatao 100,000, ili kuonyesha mshikamano kwao akiwataka wafahamu kwamba hayuko tofauti nao katika furaha, matumaini na huzuni zao.

Comments are closed.