PAPA FRANCIS AZURU MSIKITI WA BANGUI AFRIKA YA KATI

PAPA FRANCIS AZURU MSIKITI WA BANGUI AFRIKA YA KATI

Like
347
0
Monday, 30 November 2015
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.

Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya wakristu na waislamu.

Papa Francis alikutana na waislamu waliokwama katika sehemu ya mji unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa Kikristu waliojihami vikali wa Anti-Balaka.

Comments are closed.