PAUL RYAN ATEULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE MAREKANI

PAUL RYAN ATEULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE MAREKANI

Like
189
0
Friday, 30 October 2015
Global News

MWANASIASA wa chama cha Republican nchini Marekani Paul Ryan ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani.

Ryan, anayetoka jimbo la Wisconsin, hakutaka kuwania mwanzoni lakini mwisho alijitosa kwenye kinyang’anyiro na kuungwa mkono na wengi wa wabunge wa Republican katika Bunge la Congress kumrithi John Boehner aliyetoka Ohio.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa mgombea mwenza wa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican Mitt Romney mwaka 2012.

Comments are closed.