PELLEGRINI KUTETEA KIBARUA CHAKE LEO

PELLEGRINI KUTETEA KIBARUA CHAKE LEO

Like
267
0
Sunday, 12 April 2015
Slider

Mwalimu wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesisitiza kuwa klabu yake hiyo haina mgogoro.

Pellegrini ambae ni raia wa Chile atakuwa na kibarua kikgumu leo kutetea kibarua chake kisiote nyasi pindi klabu hiyo itakaposhuka dimbani kuchuana vikali na Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford

Manchester City imeshuka hadi nafasi ya nne kufuatia msururu mbaya wa matokeo baada ya kushinda mara mbili pekee kati ya mechi saba.

Pellegrini

Kocha Pellegrini amewaona wapinzani wake Arsenal na Manchester United wakipanda katika jedwali katika majuma ya hivi karibuni na sasa anajua kwamba atasalia kuwa mkufunzi wa kilabu hiyo iwapo atafanikiwa kuiweka timu hiyo katika nne bora zitakazofuzu katika mashindano ya kuwania kilabu bingwa Ulaya msimu ujao.

 

Comments are closed.