PINDA AWATAKA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU

PINDA AWATAKA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU

Like
305
0
Monday, 17 November 2014
Local News

 

WAZIRI MKUU Mheshimiwa MIZENGO PINDA amewataka wakulima na wafugaji nchini hususani wa wilayani Kiteto mkoani Manyara kuishi kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa pamoja na kuondoa tofauti zao za ukabila ili kuondokana na migogoro ya muda mrefu na kuliletea Taifa maendeleo.

Waziri PINDA ametoa wito huo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha ripoti na kauli ya serikali juu ya namna serikali inavyoendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua mgogoro huo.

Mbali na hayo pia mheshimiwa Pinda amesema kuwa serikali imejiwekea mikakati madhubuti katika kutatua suala hilo ikiwemo kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya ardhi kwa kuishirikisha Wizara husika.

 

Comments are closed.