PINDA: TANZANIA BILA FOLENI INAWEZEKANA

PINDA: TANZANIA BILA FOLENI INAWEZEKANA

Like
274
0
Thursday, 27 November 2014
Local News

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA amesema kuwa serikali imedhamiria kuondoa tatizo la msongamano  wa magari katika miji yote mikubwa ikiwemo Dar es salaam, Mwanza na Arusha kwa kuwashirikisha wananchi pamoja na vyombo husika kupitia sheria na Taratibu zilizowekwa.

Waziri PINDA ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kilwa mheshimiwa MURTAZA MANGUNGU aliyehoji kutaka kujua mikakati ya serikali katika utekelezaji wa suala hilo nchini.

Bunge linaendelea tena leo mjini Dodoma ambapo kutakuwa na Tamko la serikali juu ya taarifa iliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma –PAC ikifuatiwa na majadiliano kutoka kwa Wabunge.

Ripoti ya Kamati hiyo imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.

 

Comments are closed.