PIS YASHINDA UCHAGUZI POLAND

PIS YASHINDA UCHAGUZI POLAND

Like
127
0
Tuesday, 27 October 2015
Global News

CHAMA cha kihafidhina nchini Poland cha sheria na haki PiS kimeshinda uchaguzi  mkuu  uliofanyika Jumapili iliyopita kwa  mujibu  wa  matokeo  rasmi  yaliyotangazwa jana  jumatatu.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi zinasema kuwa Chama  cha  PiS  kilipata  asilimia  37.6  ya kura, huku  chama  cha  Civic Platform PO kimeshika  nafasi ya  pili kwa kupata  asilimia  24.1.

Mgawanyiko  rasmi  wa  viti  bungeni ulikuwa bado haujapatikana, lakini  wadadisi  wanasema  matokeo huenda  yakatoa kwa  chama  cha  PiS, ukiwa  ni  ushindi  mkubwa kwa  chama  kimoja  tangu Poland  kuachana  na  siasa  za  kikomunist  mwaka  1989.

Comments are closed.