PLATINUM FC YAIPONGEZA YANGA KWA USHINDI WA 8-0 DHIDI YA COASTAL UNION

PLATINUM FC YAIPONGEZA YANGA KWA USHINDI WA 8-0 DHIDI YA COASTAL UNION

Like
343
0
Thursday, 09 April 2015
Slider

Katika michezo ya ligi iliyochezwa jana Yanga imeifunza adabu ya timu ya Coastal Union kwakuitandika magoli 8-1.

Huenda Yanga iliutumia mchezo huo kama salamu kwa vigogo wa Tunisia Etoile du Sahel, ambao siku za usoni watakutana katika kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo hadi mapumziko Yanga ilikuwa mbele kwa magoli 3-0.

Katika kiindi cha pili cha mchezo Amisi Tambwe alifunga magoli 4, huku Simon Msuva, Salem Telela na Mliberia Kpah Sherman wakiona nyavu pia.

Akizungumza na efm kocha wa yanga amesema hakutarajia kama wangetoa kichapo hicho ila alitarajia ushindi kwa timu yake

Kupitia mtandao wa twitter pia timu ya Platinum fc imeipongeza Yanga kwa ushindi huo

Kwa ushindi huo wa jana yanga inaongoza kwa pointi 43 kwenye msimamo wa ligi kuu huku nyuma yao wakifuatiwa na mabingwa watetezi wa Azam ambao pia walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City wakiwa na pointi 37

Comments are closed.