POLISI KENYA YAKAMATA MABOMU KWENYE MISIKITI INAYODAIWA KUTOA MAFUNZO YA ITIKADI KALI

POLISI KENYA YAKAMATA MABOMU KWENYE MISIKITI INAYODAIWA KUTOA MAFUNZO YA ITIKADI KALI

Like
355
0
Monday, 17 November 2014
Global News

 

POLISI nchini Kenya wanasema kuwa wamenasa mabomu ya kurusha na silaha mbalimbali usiku wa kuamkia leo katika msako mkali walioanza kufanya dhidi ya misikiti inayodaiwa kutoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini Mombasa Pwani ya Kenya.

Mtu mmoja ameuawa na wengine zaidi ya 250 kukamatwa katika msako huo unaolenga misikiti inayosemekana kutoa mafunzo kuhusiana na harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Al Shabaab nchini Somalia.

Polisi wanadai kuwa misikiti hiyo ikiwemo Masjid Musa inatumika kwa kuwasajili vijana wanaojiunga na Al Shabaab nchini Somalia.

Msikiti mwingine uliolengwa ni ule wa Sakina.

 

Comments are closed.