POLISI KUCHUNGUZA KIFO CHA DADA WA BILIONEA MSUYA

POLISI KUCHUNGUZA KIFO CHA DADA WA BILIONEA MSUYA

Like
453
0
Monday, 30 May 2016
Local News

JESHI la polisi kanda maalumu ya Dar es salaamu limethibitisha kuundwa kwa timu maalumu kwa ajili ya kuchunguza na kupeleleza kifo cha dada wa bilionea Msuya ambapo tayari wanamhoji aliyekuwa mume wake .

 

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi kanda hiyo, kamishina  SIMON  SIRRO, Jeshi hilo pia limefanikiwa kutoza faini a magari yanayo kiuka sheria za usalama barabarani ambapo kiasi cha shilingi milino 548 laki 1 na sitini  zimeweza kukusanywa.

 

Kamanda SIRRO  amewaambia wandishi wa Habari leo kuwa jeshi hilo limeendelea na oparesheni zake za kupambana na uhalifu ikiwemo uhalifu wa kutumia silaha  huku likifanikiwa kukamata watuhumiwa mbalimbali wakiwemo  majambazi ,panya roadi 26 ,dada poa na kaka poa 23.

Comments are closed.