POLISI KUCHUNGUZWA KWA TUHUMA ZA KUGAWANA FEDHA ZA VIKOBA

POLISI KUCHUNGUZWA KWA TUHUMA ZA KUGAWANA FEDHA ZA VIKOBA

Like
293
0
Wednesday, 25 February 2015
Local News

KAMISHINA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SULEIMAN KOVA ametoa agizo kuchunguza tuhuma za askari wake wanaodaiwa kugawana fedha shilingi milioni Nane ambazo zilikuwa Mali za Akina Mama Wajasiriamali waliojiunga kwenye vikoba.

KOVA ameeleza hayo jijini Dar es salaam na kusema kuwa tuhuma hizo amezesikia lakini hawezi kumhukumu mtu hivyo ametoa agizo kuwa uchunguzi ufanyike.

Amebainisha kuwa endapo uchunguzi utafanyika na kubaini kuwa askari au mtu yoyote amehusika kuchukua fedha hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Comments are closed.