POLISI LONDON WAPEKUA MSIKITI KUCHUNGUZA MAUAJI YA IMAM WA SYRIA

POLISI LONDON WAPEKUA MSIKITI KUCHUNGUZA MAUAJI YA IMAM WA SYRIA

Like
255
0
Wednesday, 15 April 2015
Global News

POLISI mjini London wamekuwa wakiupekua msikiti mmoja ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wake wa mauaji ya Imam mmoja wa zamani kutoka Syria.

Abdul Hadi Arwani alipigwa risasi na kuuawa wiki moja iliopita katika makazi ya Wembley mjini London.

Msemaji wa polisi amesema kuwa maafisa wamekuwa wakiwasiliana na wawakilishi wa jamii ya waislamu ili kuwahakikishia kwamba upekuzi huo  ni muhimu, na kwamba msikiti huo utafunguliwa haraka iwezekanavyo.

Abdul Arwani ameripotiwa kuwa mpinzani wa rais Assad wa Syria.

Watu wawili wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.

 

 

Comments are closed.