POLISI WAPAMBANA NA AL SHABAAB KASKAZINI MASHARIKI MWA KENYA

POLISI WAPAMBANA NA AL SHABAAB KASKAZINI MASHARIKI MWA KENYA

Like
246
0
Tuesday, 26 May 2015
Global News

ASKARI mmoja ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati ya Polisi na wanamgambo wa Al Shabaab Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Kenya

Wizara ya usalama wa Taifa nchini Kenya kupitia kwa msemaji wake MWENDA NJOKA imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la wanamgambo hao  katika kijiji cha Yumbis.

Wakati huo huo AL SHABAAB wamekiri kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20 lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo sio ya kweli.

Comments are closed.