POLISI YAJIANDAA KUZUIA MAANDAMANO YA VIJANA WAHITIMU WA JKT

POLISI YAJIANDAA KUZUIA MAANDAMANO YA VIJANA WAHITIMU WA JKT

Like
1103
0
Tuesday, 17 February 2015
Local News

JESHI la Polisi limesema wamejiandaa na lipo tayari kuzuia maandamano yaliyopangwa kufanywa na baadhi ya ya vijana Zaidi ya 200 waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa-JKT kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2013.

Tayari Vijana hao kutoka mikoa mbalimbali nchini wametangaza kuwa watafanya maandamano makubwa kwa siku tatu katika jiji la Dar es salaam kwa lengo la kwenda Ikulu kumuona Rais KIKWETE ili kumweleza shida zao ikiwemo ya kutokuwa na ajira ya kudumu tangu wamalize mafunzo hayo.

Pia vijana hao wameeleza kuwa wamepata mafunzo ya kutosha ya kijeshi hivyo iwapo maandamano yao yatazuiliwa wapo tayari kupambana.

Comments are closed.