POLISI YAPANGA KUIMARISHA ULINZI TEMEKE KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU

POLISI YAPANGA KUIMARISHA ULINZI TEMEKE KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU

Like
311
0
Thursday, 16 July 2015
Local News

JESHI la Polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke limesema kuwa limejipanga kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote katika kipindi hiki cha sikukuu kuanzia katika maeneo ya Ibada.

Akizungumza na Efm kamanda wa Polisi mkoa huo Andrew Satta amewataka wananchi kudumisha ulinzi wa mali zao katika kipindi hiki cha sikukuu ya Iddy el fitri.

Kamanda Satta amewataka wananchi kutojisahau na kuacha nyumba zikiwa zimefungwa na badala yake waache mtu mzima ili kuzuia vitendo vya uhalifu.

 

Comments are closed.