POLISI YATAKIWA KUWAJALI WAZEE NA WATOTO

POLISI YATAKIWA KUWAJALI WAZEE NA WATOTO

Like
225
0
Friday, 18 September 2015
Local News

JESHI la polisi nchini limetakiwa kuwajali watoto na wazee wakati wa kuzuia vurugu zinapotokea kwa kuwa makundi hayo ya watu ndio huaathirika zaidi.

Akizungumza na kituo hiki mmoja wa wazazi anayefahamika kwa jina la Agatha Kadaso ambaye mtoto wake amejeruhiwa jicho kwa bomu la machozi wakati wa kutuliza vurugu kati ya jeshi la polisi na madereva wa daladala wilaya ya Misungwi amesema jeshi hilo linapaswa kuzingatia usalama wa watoto na wazee kwa makini.

Comments are closed.