PRINCE ALI BIN AL AL HUSSEIN AMTAKA BLATTER KUTOJIHUSISHA NA MAGEUZI FIFA

PRINCE ALI BIN AL AL HUSSEIN AMTAKA BLATTER KUTOJIHUSISHA NA MAGEUZI FIFA

Like
241
0
Thursday, 23 July 2015
Slider

Mwanamfalme Ali bin Al Hussein wa Jordan, aliyeshindwa uchaguzini na Sepp Blatter jaribio lake la kutaka kuwa rais wa Fifa mwezi Mei, amesema Blatter hafai kusimamia shughuli ya mageuzi kwenye shirikisho hilo lililoandamwa na kashfa ya ufisadi.

Amesema jukumu hilo linafaa kuachiwa mrithi wake.

Kupitia taarifa iliyotolewa Jumatano, Mwanamfalme Ali, aliyejiondoa uchaguzini duru ya pili baada ya kupata kura 73 dhidi ya 133 za Blatter duru ya kwanza, alisema ana wasiwasi Blatter, ambaye ameongoza shirikisho hilo linalosimamia soka duniani tangu 1998, anajaribu kuharakisha mageuzi kabla yake kuondoka rasmi afisini Februari 26.

Blatter alitangaza angejiuzulu kutoka wadhifa huo siku chache tu baada ya kuchaguliwa tena kutokana na kashfa iliyosababisha kushutumiwa sana kwa uongozi wake.

“Tunahitaji shughuli wazi, iliyoelezwa vyema na tarehe kuweka. Haya yote yanafaa kutekelezwa na rais mpya,” akasema Mwanamfalme huyo, ambaye bado hatangaza iwapo atawania tena kwenye uchaguzi huo wa Februari.

“Ingawa mageuzi hayo yanahitajika sana, yanafaa kutekelezwa na rais mpya, si yule wa zamani.

“Ni jukumu la rais mpya kuweka mifumo ifaayo ya kutekeleza mabadiliko ambayo Fifa inahitaji sana, si Jopokazi linalotaka kuharakisha hili na kulikamilisha katika chini ya siku 60,” akaongeza.

Fifa iliyumbishwa Mei watu tisa walio au walikuwa maafisa wa zamani wa kusimamia soka, wengi ambao walikuwa na vyeo vikubwa Fifa, pamoja na maafisa watano wa mauzo na utangazaji, waliopotuhumiwa kushiriki kashfa ya kutoa na kupokea hongo, ulanguzi wa pesa na ulaghai na maafisa wa Marekani.

Jumatatu, Blatter alitangaza Fifa itaunda jopo kazi la watu 10 kutoka mashirikisho sita ya mabara ya Fifa na ‘mwenyekiti asiyeegemea upande wowote’ ambalo litashughulikia mageuzi katika shirikisho hilo.

Comments are closed.