PRO. TIBAIJUKA: KAMWE SITAJIUZULU

PRO. TIBAIJUKA: KAMWE SITAJIUZULU

Like
370
0
Thursday, 18 December 2014
Local News

WAZIRI wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe Profesa Anna Tibaijuka amesema kamwe hawezi kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow kwa kuwa hausiki na wizi wa fedha hizo na kusema kuwa kama akijiuzulu atakuwa hatendei haki dhana ya kuchakalika ili kuleta maendeleo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dare s salaam Tibaijuka amesema kuwa fedha aliyoipokea ni mchango wa shule katika taasisi ya Shirika la JOHA TRUST wa shilingi Bilioni moja milioni mia 6 kumi na saba na laki moja kutoka kwa bwana James Rugemalira wa VIP engineering and market limited kwa ajili ya kuendeleza elimu kwa watoto wa kike hapa nchini.

Aidha amesema kuwa kwa kuwa walihakikishiwa na Benki ya Mkombozi kwamba fedha za bwana Rugemalira zilikuwa zimelipwa kodi waliweza kupokea mchango wake kwa furaha bila wasi wasi wowote-DEC-18-TIBAIJUKA 1.

Hata hivyo Waziri Tibaijuka amekanusha usemi kuwa yeye si kiunganishi wa fedha za ESCROW na kusema kuwa yeye na profesa muhongo wanafahamiana na hawawezi kuacha kuongea kwa kuwa wote ni mawaziri ambao Raisi kikwete amewaamini -DEC-18-TIBAIJUKA 2.

Comments are closed.