PROF. LIPUMBA AJIENGUA UWENYEKITI CUF

PROF. LIPUMBA AJIENGUA UWENYEKITI CUF

Like
207
0
Thursday, 06 August 2015
Local News

MWENYEKITI wa chama cha wananchi –CUF, Profesa Ibrahim Lipumba leo ametangaza rasmi kujiengua nafasi hiyo kutokana na umoja wa katiba ya wananchi –UKAWA, kushindwa kuenzi na kuzingatia tunu za Taifa juu ya rasimu ya katiba pendekezwa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam, Profesa Lipumba ameeleza kuwa tunu hizo ni pamoja na kushindwa kufahamu utu wa watanzania juu ya kuipata katiba pendekezwa uzalendo, uadilifu umoja, uwazi na uwajibikaji.

 

Amefafanua kuwa kutokana na maudhui ya rasimu ya katiba waliyoipinga ndani ya bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kuwekwa kando na umoja  huo hali hiyo imemfanya dhamira yake kumsuta na kuona hatalitendea taifa haki kama ataendelea kuwa mwenyekiti wa CUF.

 

Comments are closed.