PROF: LIPUMBA KUSIMAMA KIZIMBANI

PROF: LIPUMBA KUSIMAMA KIZIMBANI

Like
261
0
Wednesday, 28 January 2015
Local News

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es salaam, imelazimika kumpeleka Kituo cha afya cha UN, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi –CUF , Profesa Ibrahim Lipumba, baada ya kupatwa na mshituko wa Moyo akiwa katika mahojiano na polisi kuhusiana na maandamano yaliyokuwa yafanywe na chama hicho jana.

Kwa mujibu wa Mwandishi wetu anayefuatilia tukio hilo, Hali ya Profesa Lipumba inaendelea vizuri na tayari amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu ambako anatarajiwa kusomewa mashitaka yake.

Hapo jana Profesa Lipumba pamoja na baadhi ya viongozi wa chama hicho waliwekwa kizuizini makao Makuu ya Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam, kwa madai ya kuandaa na kufanya maandamano bila kibali cha kuruhusiwa kufanya hivyo.

Comments are closed.