PROF. MBARAWA: SERIKALI BADO INA MASHAKA NA WATENDAJI ATCL

PROF. MBARAWA: SERIKALI BADO INA MASHAKA NA WATENDAJI ATCL

Like
238
0
Monday, 15 February 2016
Local News

WAZIRI wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa  Makame Mbarawa amesema Serikali bado ina mashaka na watendaji wa shirika la ndege la taifa ATCL na ili kuondoa dukuduku hilo inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watendaji wote waliohusika kulihujumu shirika hilo.

Profesa Mbalawa ameyasema hayo jijini Mwanza kwenye mkutano wa sita wa sekta ya uchukuzi  katika ukanda wa Afrika ya kati kwa lengo la kutathmini maendeleo katika sekta hiyo pamoja na changamoto zake  uliowakutanisha mawaziri wa sekta hiyo kutoka nchi tano za ukanda huo.

leongo kubwa la mkutano huo ni kuondoa vikwazo wakati wa usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani.

Comments are closed.