PROFESA ALIEMBEBA MTOTO WA MWANAFUNZI WAKATI WA MTIHANI AJIZOLEA UJIKO

PROFESA ALIEMBEBA MTOTO WA MWANAFUNZI WAKATI WA MTIHANI AJIZOLEA UJIKO

Like
462
0
Wednesday, 29 June 2016
Global News

Profesa mmoja wa chuo kikuu amesifiwa nchini Ivory Coast kwa kumbeba mtoto wa mmoja wa wanafunzi wake mgongoni wakati wa masomo.

Picha za Honore Kahi wa chuo cha Bouake, zimesambaa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema aliamua kumsaidia mwanamke katika darasa lake wakati mtoto alianza kulia.

Picha zilizochukuliwa na mwanafunzi mwingine zinamuonyesha, bwana Kahi akifunza huku mtoto akiwa mgongoni.

Comments are closed.