PROFESA MUHONGO: MILANGO YA UWEKEZAJI IKO WAZI KWA MATAIFA YOTE KUWEKEZA TANZANIA

PROFESA MUHONGO: MILANGO YA UWEKEZAJI IKO WAZI KWA MATAIFA YOTE KUWEKEZA TANZANIA

Like
305
0
Tuesday, 22 March 2016
Local News

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa milango ya uwekezaji iko wazi kwa Mataifa yote duniani yenye nia thabiti ya kufanya hivyo nchini Tanzania.

 

Profesa Muhongo ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati wa kikao chake na Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku ambaye alifika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kufahamu zaidi nafasi za uwekezaji kwa ajili ya manufaa ya Kampuni za uwekezaji za Afrika Kusini.

 

Katika kikao hicho, Profesa Muhongo amemueleza Balozi Mseleku kuwa Tanzania ina nafasi nyingi za uwekezaji katika masuala ya Nishati na kutaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na makaa ya mawe na umeme wa jua.

MGOMBEA Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican nchini Donald Trump amesema kuwa akichaguliwa kuwa Rais hatua ya kwanza atakayochukua juu ya masuala ya mambo ya nje ni kuuvunja mkataba wa nyuklia.

Mkataba huo ambao Trump anauzungumzia na kukerwa nao ni ule wa Marekani na Iran.

Trump, ambaye kwa sasa yuko mstari wa mbele katika kinyang’anyiro hicho katika chama chake ameliambia kundi lenye ushawishi mkubwa linalounga mkono Israel kuwa mapatano hayo ya Iran ni hatari kwa Marekani.

Comments are closed.