RAIS wa Urusi Vladimir Putin ametetea uamuzi wa nchi yake wa kuchukua hatua za kijeshi nchini Syria, kwa kusema kuwa lengo lake ni kusaidia utawala halali wa Rais wa Syria Bashar al-Assad.
Awali rais Putin aliiambia runinga ya taifa ya Urusi kwamba Moscow pia inataka kuunda mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa maafikiano ya kisiasa nchini humo.
Hata hivyo amekanusha madai kwamba mashambulio ya ngani ya Urusi yanalenga makundi ya upinzani badala ya yale ya wapiganaji wa Islamic State.