RAGE AWACHANA NA KUWAPA USHAURI CECAFA, AWAKINGIA KIFUA YANGA

RAGE AWACHANA NA KUWAPA USHAURI CECAFA, AWAKINGIA KIFUA YANGA

Like
612
0
Friday, 06 July 2018
Sports

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amewashauri CEFACA kutoyachukulia mashindano ya KAGAME kama bonanza na badala yake yafuate ratiba.

Rage ambaye aliwahi kuiongoza Simba kabla ya ujio wa utawala wa Evans Aveva, amewashauri CECAFA kupitia Katibu Mkuu wake, Nicholas Musonye wajipange upya ili kuondoa mkanganyiko kwa klabu za ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Radio EFM, auli ya Rage imekuja kufuatia baadhi ya klabu kujiondoa kutokana na ratiba ambayo haikuwa si rafiki kwao ikiwemo Yanga ambayo inajiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kiongozi huyo amesema hata kama CECAFA wangeiadhibu Yanga wangekuwa wanaionea bure kutokana na mashindano yenyewe kufanyika bila kalenda maalum ambayo imekuwa haifuati uwepo wa ratiba za mashindan mengine.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Simba, amewashauri CECAFA ikifike hatua sasa wayapangia ratiba maalum na ijulikane ili yaweze kuziandaa timu vizuri kuelekea klabu bingwa Afrika na hata kombe la shirikisho, badala ya kutafanya kama bonanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *