RAIA WA AUSTRALIA WAKABILIWA NA ADHABU YA KIFO BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

RAIA WA AUSTRALIA WAKABILIWA NA ADHABU YA KIFO BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

Like
199
0
Wednesday, 04 March 2015
Global News

WATU  wawili  raia  wa  Australia  waliopatikana  na  hatia  ya kusafirisha  dawa  za  kulevywa   wamehamishwa   kutoka  jela mjini  Bali  nchini  Indonesia  leo  na  kupelekwa  katika  kisiwa kimoja  nchini  humo  ambako  watauwawa  kwa  kupigwa  risasi.

Kwa  mujibu  wa  ripoti  za  vyombo  vya  habari  nchini  Australia, hatua  hiyo  ya  adhabu  ya  kifo  kwa  Myuran Sukumaran  na Andrew Chan imeongeza  wasiwasi  wa  kidiplomasia,  huku  kukiwa na  maombi  ya  msamaha  kwa  watu  hao  wawili  kutoka  Australia, na imeiweka Indonesia  katika  hali  ya  kuonekana  kuwa  inatumia adhabu  ya  kifo  kwa  raia  wa kigeni.

Chan  na  Sukumaran  walihukumiwa  mwaka  2005  kama  viongozi wakuu  wa  genge  linalojulikana  kama  Bali Nine, ambao walikamatwa  katika  uwanja  wa  ndege  wa  Denpasar  kwa kujaribu  kusafirisha  kilo  8  za  mihadarati  kwenda  Australia.

 

Comments are closed.