RAIA WA BURUNDI WAGOMA KUREJEA NCHINI KWAO LICHA YA KUREJEA KWA AMANI

RAIA WA BURUNDI WAGOMA KUREJEA NCHINI KWAO LICHA YA KUREJEA KWA AMANI

Like
236
0
Friday, 29 May 2015
Local News

WAKATI Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Kimataifa -UN wakijiandaa kuwarudisha wakimbizi walioingia nchini kutoka Burundi mara baada ya hali ya usalama kupatikana, wakimbizi hao wamesema kuwa hawako tayari kurudi nchini humo kwa madai kuwa burundi siyo nchi ya kulinda amani kwa wakati wote.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakimbizi hao wamesema kuwa Serikali ya burundi haiaminiki hata kidogo kwani kila mara nchi hiyo imekuwa na migogoro ya hapa na pale  inayosababisha mauaji ya aina mbalimbali ndani ya jamii.

Comments are closed.