RAIA WA KUWAIT AKAMATWA NA KENGE 149 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JK NYERERE

RAIA WA KUWAIT AKAMATWA NA KENGE 149 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JK NYERERE

Like
398
0
Friday, 09 January 2015
Local News

POLISI WA UWANJA wa Ndege wa Kimataifa  wa Julias Nyerere-JNIA wamefanikiwa kumkamata Raia wa Kuwait,HASSAIN AHMED ALLY kwa tuhuma za kukutwa na Viumbe aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Shilingi Milioni 6 nukta kinyume cha sheria .

Kamanda wa Polisi wa Uwanjani hapo HAMISI SELEMAN amesema kuwan raia huyo amekamatwa na Kenge hao ambao amewaweka katika   mifuko midogo midogo iliyokuwa kwenye  begi lake  kubwa.

Amesema kuwa tukio hilo limetokea wakati HASSAN akijiandaa na  safari ya  kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai na  Shirika la Emirates ingawa kati ya Kenge hao 15 walikufa huku hai wakiwa 134 .

Comments are closed.